Category: Local News

  • ALICHOSEMA KIKWETE BAADA YA KUKUTANA NA RAIS MAGUFULI IKULU LEO

    ALICHOSEMA KIKWETE BAADA YA KUKUTANA NA RAIS MAGUFULI IKULU LEO

    Mhe. Rais John P amagufuli akiwa na Rais mstaafu Mhe. J Kikwete
    “Nimekuja kumsalimia nakumtakia kila la heri, anafanya kazi nzuri, aendelee tu kuchapa kazi na sisi tupo kwa namna yoyote ya kumpa nguvu, tupo tayari kumsaidia” amesema Mhe. Rais Mstaafu Kikwete.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 23 Oktoba, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
    Baada ya mazungumzo yao Mhe. Rais Mstaafu Kikwete amesema wamekutana kwa utaratibu wa kawaida wa kusalimiana na kutakiana heri katika majukumu.
    Aidha, Mhe. Rais Mstaafu Kikwete amebainisha kuwa Mhe. Rais Magufuli anafanya kazi nzuri na amemtaka aendelee hivyo hivyo

  • January Makamba ahusishwa sakata mo

    January Makamba ahusishwa sakata mo

    Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumhoji kwa saa kadhaa na kumwachia Waziri January Makamba kuhusiana na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji. Kupitia ukurasa wake wa Twitter waziri huyo ameandika, hajakamatwa na polisi na kuwa yupo salama.

    “Polisi walinipigia simu kuniomba, kama rafiki wa Mohamedi Dewji, niwasaidie kama kuna chochote cha ziada ambacho Mo aliniambia kinachoweza kusaidia uchunguzi. Niliwaeleza wakasema kinafanana na alichowaeleza, wakanishukuru. Wamefanya hivi pia kwa wanafamilia. Sikukamatwa”. amesema J.Makamba

  • mo dewji apatikana usiku wa manane

    mo dewji apatikana usiku wa manane

    Afisa mkuu wa polisi wa kanda ya Dar es salaam Lazaro Mombasa aliyetembelea nyumbani kwao Dewji kuthibitisha kurejea kwake nyumbani, watu waliomkamata walikuwa na lafudhi ya mojawapo ya lugha za mataifa ya Afrika Kusini. Aliongezea kwamba hatua hiyo imethibitisha wazi kwamba waliomteka sio watanzania.

    Mo Dewji; Ninawashukuru Watanzania kwa kuniombea

    ”Nataka kuuthibitishia umma wa Tanzania kwamba nimefika nyumbani kwa akina Mo Dewji nimeongea naye niko na kikosi cha makachero hapa na ndugu yetu ni mzima kama IGP alivyozungumza na umma kwamba jeshi la polisi litaendelea na uchunguzi ili kuhakikisha kwamba tunampata muhusika akiwa mzima.

    Mo Dewji ambaye alionekana mchovu alimshukuru mwenyezi mungu na serikali ya rais Pombe Magufuli pamoja na Watanzania kwa kumuombea.

    ”Namshkuru mwenyezi mungu , serikali ya magufuli na IGP , ahsanteni mimi ni mzima nawashukuru Watanzania wote kwa kuniombea.

    Babake Mo alivimbia vyombo vya habari kwamba mwendo wa saa nane alifajiri walipokea simu ya Mo kwamba yuko salama na moja kwa moja wakaelekea katika eneo la Gymkhana ambako alikuwa amewachwa na watekaji wake.

    ” Tumshukuru mwenyezi Mungu kwamba tumempata salama na anaendelea vizuri. Walikuwa wamemuacha pale na kuondoka. Lakini alikuwa hajafungwa na yuko sawasawa. Tunawashukuru Watanzania wote na rais”.

  • Igp sirro afunguka kuhusu mo dewji; gari lahusiswa

    Igp sirro afunguka kuhusu mo dewji; gari lahusiswa

    Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro amesema polisi  wamepata maelezo muhimu kuhusu gari lililotumiwa na watu waliomteka mfanyabiashara Mo Dewji.

    Amesema gari hilo lilitokea nchi jirani ambayo hakuitaja na kueleza kuwa liliingia nchini Tanzania mnamo 1 Septemba, amewaonesha wanahabari picha za gari hilo ambapo amesema wanaomba maelezo zaidi.

    Kamanda Sirro amesema wanafuatilia kwa pamoja na polisi wa kimataifa wa Interpol.

    Amesema kufikia sasa hawafahamu iwapo gari hilo bado lipo Tanzania na akawaomba wananchi kutoa taarifa kwa polisi wakiliona.

    “Tumefuatilia na watu wetu wamekwenda mpaka mpakani na wameweza kuona lilipita 1 Septemba 2018. Tumepata maelezo ya kutosha ambayo siwezi kuyasema,” amesema.

    Sirro amesema kwa kutumia kanda za kamera za CCTV wamebaini kwamba gari hilo aina ya Surf baada ya kutoka hoteli ya Colosseum, lilipita Hassan Mwinyi, mpaka maeneo mzunguko wa barabara ya kwenda Kawa.

     

    “Bado watu wetu wanafuata kuonelea kama walielekea maeneo ya SilverSand au Kawa,” amesema.

    “Hapo tunaamini gari hilo lilipotelea, tunakwenda jumba kwa jumba kutafuta.”

    “Tumehakikisha pia kuna watu wetu watazunguka baadhi ya nchi hizo jirani.”

    Kuhusu usaidizi kutoka nje, Kamanda Sirro amesema: “Tukiona kuna hiyo sababu tutamshauri Amiri jeshi Mkuu mheshimiwa Rais. kwa hali tuliyo nayo sidhani kama ipo sababu,” amesema Sirro.

    Kamanda Sirro amepuuzilia mbali taarifa kwamba kuna uwezekano kamera za CCTV ‘zilichezewa’ na kwamba hazikuwa zinafanya kazi wakati wa tukio.

    “Ile kanda haikuwa wazi sana kwa sababu ya wakati huo (asubuhi na mapema) na aliyekuwa anaifuatilia kwa wakati huo, lakini baadaye kwa kuunganisha maelezo mbalimbali, unaweza kupata maelezo,” amesema Sirro.

    “Kama ilikuwa haifanyi kazi, hizo kanda ambazo hazikuwa wazi zilipatikana vipi?”

    Watuhumiwa wanaoshikiliwa na polisi

    Kamanda Sirro amesema kufikia sasa watu wanazuiliwa na polisi kuhusiana na kisa cha kutekwa kwa Mo.

    Amesema watu wengine takriban 26 ambao walikuwa wanahojiwa wameachiliwa huru.

    Mkuu huyo amesema kufikia sasa bado hawezi kubaini iwapo tajiri huyo aliyetekwa yuko hai au la.

    Amewahimiza watu walio na uwezo wa kumiliki silaha kwa njia halali kufanya hivyo, na kusema ingawa taifa hilo ni salama ni vyema kuzingatia usalama wao.

    Sirro amesema huenda Watanzania wasiwe hatari kwao lakini kukawa na watu wenye nia mbaya kutoka nchi nyingine.

    Amewataka pia wananchi kutofautisha kati ya mtu kupotea na kutekwa.

    Amesema wapo watu wanaotoroka makwao kwa hiari na kurejea baada ya miaka mingi.

    “Nikitoka nikamwacha mke wangu nikaenda Marekani, mtasema IGP katekwa?” amesema.

  • hizi ndizo sababu za Rais magufuli kutokutoa dream liner

    hizi ndizo sababu za Rais magufuli kutokutoa dream liner


    Picha kutoka Ikulu Dar Es Salaam mahali ambapo Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Oktoba, 2018 anakutana na wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) na baadaye kula nao chakula cha mchana.

    Hii nikufuatia Timu ya Taifa (taifa stars) kushinda mechi dhidi ya Cape Verde iliyochezwa mwanzoni mwa wiki hii,  mchezo huo ulimalizika taifa stars 2 – Cape Verde 0 magoli yalifungwa na Mbwana Sammatta na Simon Msuva.

    Pia Raisi Magufuli amezugumza na timu ya taifa na amesema “Mh Waziri alipokuwa akitafuta ndege nilikuwa nipo kwenye ‘stage’ ya mwisho kutoa ndege bure baadae nikaambiwa ule uwanja hautoshi kwa ndege ya Dream Liner kutua lakini nilivyoanza kufuatilia ule mchezo dakika chache tu mmeshatandikwa wakati mnaenda mapumziko nikasema ni nafuu uwanja ule umekuwa mfupi ndge yangu sikutoa”.

  • Lugola amesimikwa kuwa Chifu

    Lugola amesimikwa kuwa Chifu

    Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesimikwa kuwa Chifu wa kabila la Wasafwa kutoka mkoani Mbeya kama ishara ya kupambana na adui atakaekuja mbele yake.

     

  • sakata la kutekwa kwa mo dewji giza nene

    sakata la kutekwa kwa mo dewji giza nene

    Tukio la kutekwa bilionea Mohammed Dewji, 43, Alhamisi ya wiki iliyopita bado limesalia kuwa ni fumbo lisilokuwa na jibu.

    Mpaka kufikia leo bado haijulikani ni akina nani waliomteka na wapi walipomficha na lipi hasa kusudio la kumteka mfanya biashara huyo maarufu kama Mo.

    Mo alikwapuliwa na watu wasiojulikana nje ya hoteli moja jijini Dar es Salaam alipokuwa akienda kufanya mazoezi. Toka hapo, giza nene limetanda juu ya tukio hilo, licha ya hatua kadhaa ambazo mamlaka za nchi na familia imezichukua.

    Toka siku ya kwanza ya tukio polisi kupitia Kamanda wa Dar es Salaam wamekuwa wakiuhakikishia umma kuwa ulinzi umeimarishwa na uchunguzi unafanyika kwa kasi na weledi. Maeneo yote ya kutoka na kuingia jiji la Dar es Salaam ikiwemo fukwe za bahari zinakaguliwa.

    Hatahivyo, si wote wanaoonekana kuridhishwa na kasi ya uchunguzi. Mathalan, suala la picha za kamera za CCTV zilizonasa tukio hilo ni kizungumkuti. Polisi wanasema kamera za hoteli hazikunasa tukio hilo ipasavyo na kuwapa ugumu wa kung’amua undani wa tukio hilo.

    Hata hivyo, waziri kivuli wa mambo ya ndani na mbunge wa upinzani Godbless Lema ameonesha wasiwasi wake juu ya kauli za mamlaka akitaka picha hizo ziwekwe wazi ili wananchi wasaidie katika utambuzi wa watekaji na magari yaliyotumika.

    Gazeti la Mwananchi la jana Jumatano Oktoba 17 pia limeandika kuwa licha ya uwepo wa kamera za CCTV hotelini hapo, majengo mengi yanayoizunguka hoteli hiyo na barabara ambayo yadaiwa kutumiwa na watekaji imesheheni kamera za CCTV.

    Upinzani na watumiaji wa mitandao Tanzania pia wamekuwa wakiomba serikali ikaribishe mashirika ya upelelzi ya nje kama FBI na Scotland Yard kuja kusaidia kutatua fumbo hilo lakini serikali kupitia waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola na naibu wake Hamad Masauni wote kwa nyakati tofauti wametupilia mbali ombi hilo wakisema vyombo vya ndani vya ulinzi vinauwezo wa kutosha.

    Jumla ya watu 26 walikamatwa kutokana na tukio hilo na mpaka jana Jumanne 19 waliachiwa kwa dhamana.

    Baada ya kukaa kimya kwa siku nne, familia ya Mo ilijitokeza siku ya Jumatatu na kutangaza kuwa watatoa zawadi ya Shilingi za kitanzania bilioni moja kwa yeyote atakayewapatia taarifa zitakazofanikisha kupatikana kwa Mo.

    Msemaji wa familia hiyo, Azim Dewji amesema familia inapitiakipindi kigumu na wanashukuru kwa dua na faraja wanayopewa na Watanzania.

    Licha ya kutangazwa kwa dau hilo siku tatu zilizopita, bado mpaka sasa hajapatikana.

    Mo anakisiwa kuwa na utajiri wa $1.5 bilioni kwa mujibu wa jarida la masuala ya fedha la Forbes na kumfanya kuwa tajiri namba moja Afrika Mashariki na bilionea mwenye umri mdogo zaidi Afrika.

  • rambirambi zampeleka katibu wa ccm rumande

    rambirambi zampeleka katibu wa ccm rumande

    Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, ametoa amri ya kuwekwa rumande saa 24, Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kata ya Maanga, bwana Norasco Tibakawa kwa madai ya kula rambirambi ya shilingi 20,000.

  • Godbless Lema azungumza na waandishi kuhusu Mo Dewji

    Godbless Lema azungumza na waandishi kuhusu Mo Dewji

    Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kujiuzulu kutokana na matukio ya utekaji yanayojitokeza nchini ikiwemo la mfanyabiashara ‘Mo Dewji’. Akizungumza na wanahabari leo Oktoba 16, Lema amesema kuwa kitendo cha waziri Lugola kuzuia watu kuzungumzia matukio ya utekwaji wa watu yanayojitokeza kwa sasa hapaswi kufanya hivyo badala yake ni kung’atuka ili kupisha kashfa.
    Lema amesema kuwa serikali inatakiwa kuviruhusu vyombo vya ulinzi vya kimataifa kuisaidia Tanzania na kuchunguza mfululizo wa matukio hayo yakiwemo ya kushambuliwa kwa Lissu na kupotea kwa mwanahabari.
    “Waziri wa mambo ya ndani kakiri kwamba utekaji umekuwepo, na kuna watu wametekwa, na kuna watu wametoweka, ukiwa na hekima unang’atuka, tunaitaka serikali ifanye kila liwezekanalo mara moja kuhakikisha vyombo vya upelelezi vya kimataifa vinatupatia msaada kwenye hili haraka iwezekanavyo”, amesema Lema.

  • Wakimbiza mwenge wakutana na raisi magufuli

    Wakimbiza mwenge wakutana na raisi magufuli


    Rais John .P Magufuli akiwa na wakimbiza mwenge wa Uhuru 2018 alipokutana nao Ikulu jijini Dar Oktoba 15, akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri katika ofisi ya WM (Sera, Bunge, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jesnista Mhagama

  • MAGUFULI,KENYATTA NA MUSEVENI MAJONZI SIKU 25

    MAGUFULI,KENYATTA NA MUSEVENI MAJONZI SIKU 25

    Siku 25 za majonzi kwa Magufuli, Kenyata, Museveni. Katika kipindi cha kuanzia septemba 20 hadi oktoba 14 mwaka huu zimekuwa siku za majonzi na chungu kwa baadhi ya Marais wanaounda Jumuiya ya Afrika Mashariki akiwemo Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Kenya Uhuru Kenyata, pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

    Mhe. John P Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Katika kipindi hicho cha wiki 3, tumeshuhudia majonzi yakianzia kwa Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ambapo kulitokea ajali ya kivuko cha Mv Nyerere iliyozama katika kisiwa cha Ukara, wilayani Ukerewe huku ikishuhudiwa zaidi ya watu 200 waliokuwa wamepanda kivuko hicho wakipoteza maisha.
    Mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo viongozi wenzake kutoka Kenya, na Uganda walioneshwa kuguswa na tukio hilo na walituma salamu za rambirambi kupitia balozi zao na mitandao ya kijamii.
    Oktoba 8, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kupitia kwa balozi wake nchini Tanzania, Dkt. Dan Kazungu alichangia shilingi Milioni 125, kwa ajili ya ajali hiyo iliyotokea Septemba 20 mwaka huu.
    Oktoba 10 mwaka huu majanga yalihamia kwa nchi jirani ya Kenya kufuatia ajali ya basi katika eneo la Kericho nchini humo, ajali ambayo ilipelekea vifo vya takribani watu zaidi 50 kwa mara moja.

    Yoweri Museveni Rais wa Uganda

    Kupitia tukio hilo Rais Magufuli aliandika “nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya basi iliyotokea Kericho nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50. Nakupa pole Mhe Rais Uhuru Kenyatta, familia za marehemu na Wakenya wote. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema na majeruhi wapone haraka”.
    “Nimeshtushwa sana kwa familia za Wakenya wenzangu waliopoteza maisha yao katika ajali mbaya ya barabara huko Fort Ternan katika kata ya Kericho asubuhi hii na nawatakia wale walio hospitalini ahueni haraka.” aliandika Rais Kenyata
    Oktoba 14 kuliripotiwa vifo vya zaidi ya watu 40 katika maporomoko ya udongo yaliyotokea wilaya ya Bududa nchini Uganda na kupelekea majonzi makubwa kwa raia wa nchi hiyo.
    Rais John Magufuli alimpa pole Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kwa kuandika, “Nakupa pole Mhe. Rais Museveni na wananchi wote wa Uganda kwa kuwapoteza watu zaidi ya 40 katika ajali ya maporomoko ya udongo iliyotokea katika wilayani Bududa. Watanzania tunaungana nanyi katika kipindi hiki cha majonzi na tunawaombea majeruhi wote wapone haraka.”
    Kiujumla kwa siku 25 kuanzia septemba 20 hadi oktoba 14 zimekuwa siku za majonzi na chungu kwa viongozi wa nchi hizo pamoja na raia wake kutokana na maafa yaliyotokea.

    Uhuru Muigai Kenyatta Rais wa kenya