Familia ya mfanyabiashara wa Tanzania Mohammed Dewji imetangaza zawadi nono ya shilingi billioni moja kwa yeyote atakaetoa taarifa muhimu zitakazofanikisha kupatikana kwa mfanyabiashara huyo alietekwa.
Category: Local News
-

Erasto Nyoni kuitwa taifa stars
Nyota wa Simba SC Erasto Nyoni ameitwa kikosi cha Taifa Stars kitachoshuka dimbani jumanne ijayo kucheza mechi ya Marudiano na Cape Verde katika mbio za kwenda Cameroon kucheza AFCON 2019.
Nyoni anachukua nafasi ya Hassan Kessy ambaye ataukosa mchezo huo kwa kuwa na kadi mbili za njano.
-

Mambosasa asema wanawahoji 26 kutekwa kwa Mo Dewji
-

Oktoba 14 ni maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa.
-

Mfanyabiashara Mohamedi Dewji ametekwa na watu wasiojulikana jijini das es salaam
Mfanyabiashara Mohamedi Dewji ametekwa na watu wasiojulikana leo asubuhi wakati akienda kufanya mazoezi (gym).
Taarifa za awali zinaeleza kuwa, Watu hao walifyatua risasi angani wakati akiingia Gym nakumchukua na kuondoka nae
-

Watu 55 wafariki katika ajali ya basi Kenya wakielekea Kisumu, Magufuli atuma rambirambi
Watu 55 wamefariki dunia nchini Kenya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupata ajali kwenye barabara kuu ya Nairobi-Kisumu.
Walioshuhudia wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea leo mwendo wa saa kumi na moja alfajiri.
Ajali hiyo mbaya ilitokea katika eneo la Fort Ternan Kaunti ya Kericho.
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ni miongoni mwa waliotuma salamu za rambirambi kwa Wakenya.

-

Tanzia; Mtayarishaji maarufu wa Muziki afariki dunia
Mtayarishaji wa muziki Pancho Latino amefariki dunia.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa Pancho amefikwa na umauti kwa ajali ya maji katika kisiwa cha Mbudya jijini Dar es Salaam leo Octoba 9/2018.
Tunatoa pole kwa ndugu na jamaa na marafiki pamoja na wadau wa muziki kufuatia msiba huu.
Mungu ampuzishe ndugu yetu mahali pema peponi.(amen)
-

wananchi wagoma kupanda vivuko vya ukerewe.
Wananchi wa kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani mwanza wamegoma kupanda vivuko vya MV Sabasaba na MV Ukara na kutishia kuviponda mawe wakidai kuwa na mashaka na usalama wa vivuko hivyo.
Hii ni kufuatia kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere mapema mwezi septemba na kusababisha vifo zaidi ya 200

MV Sabasaba kivuko kinachotiliwa mashaka na wananchi Ukerewe -

wese bure dar es salaam
matukio katika picha ;
Namba ya bahati 93.7 Efm Dar es salaam inawawezesha wasikilizaji wake wa mbagala zakhem mapema leo, Kwa kugawa mafuta (petroli) bure kwa pikipiki na bajaji.
-

mtikisiko na vishindo vyaikumba 95.5 morogoro
Mtikisiko na vishindo vya wana mazoezi wa 95.5 morogoro vyasikika mapema asubuhi ya leo
MATUKIO KWA PICHA
-

Wallace Karia; mchezo wa October 12 ni Muhimu sana
“Mchezo wa October 12 ni muhimu sana kabla ya October 16, 2018 kwa hiyo sasa hivi tuangalie wa October 12 kwa sababu inabidi tukacheze kule Cape Verde halafu October 16 tunamalizia hapa Wallace Karia, Rais TFF.
Watanzania waiunge mkono Taifa Stars, Waziri Mwakyembe na serikali yetu kwa kuchangia lakini mchango huo ni nauli yao wenyewe ya kuwafikisha Cape Verde.Cape Verde tutakwenda kwa mambo mawili, tangu ndege yetu imenunuliwa mipango yake ilikuwa ni kuwa na safari za nje ya nchi. Hii itakuwa safari yake ya kwanza nje ya nchi kwa hiyo tutaweka historia lakini tutaweka historia kwenda kuishangilia timu yetu na tuweke historia ya kupata ushindi kule.
Tutaondoka October 9 usiku na alfajiri ya October 10 tutakuwa tumefika Cape Verde na jioni wachezaji watafanya mazoezi, baada ya mchezo wa October 12, usiku tutaondoka kurudi nyumbani.
Kikubwa ni kwamba, ndege haitaweza kuondoka kama haitakuwa na watu wa kutosha. Ndege ina viti 22 vya Business class ambapo tayari viti 15 vimeshalipiwa, viti 31 vya Economy class vimeshalipiwa kwa ajili ya wachezaji na benchi la ufundi.”








































