Category: Local News

  • Tuache kufanya kazi kwa mazoea;jafo

    Tuache kufanya kazi kwa mazoea;jafo

    “Naomba watanzania wawe wazalendo, Tuna kasumba sana sisi watanzania ila sio watu wote wachache ambao wao hata hawajivunii chochote na nchi yao,

    Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo

    Hii sio sawa kabisa wenzetu huwa na kasumba kwenye mambo yao na sio mambo yanayohusu nchi na maendeleo yake.”

  • Sheria ya Takwimu: Ni kweli Benki ya Dunia imezuia msaada wa $50m kwa Tanzania?

    Sheria ya Takwimu: Ni kweli Benki ya Dunia imezuia msaada wa $50m kwa Tanzania?

    Kumekuwepo na taarifa kwamba Benki ya Dunia imezuia msaada wa Dola 50 milioni za Marekani ambao ulikuwa utolewe kwa serikali ya Tanzania.

    Sababu iliyotolewa ni kwamba benki hiyo imeghadhabishwa na mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa kwenye Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015

  • Rais Dkt jp Magufuli amekataa ombi la rais mstaafu

    Rais Dkt jp Magufuli amekataa ombi la rais mstaafu

    Tanzania’s President elect John Pombe Magufuli addresses members of the ruling Chama Cha Mapinduzi Party (CCM) at the party’s sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam, October 30, 2015. Tanzania’s ruling party candidate, John Magufuli, was declared winner on Thursday of a presidential election, after the national electoral body dismissed opposition complaints about the process and a demand for a recount. The election has been the most hotly contested race in the more than half a century of rule by the Chama Cha Mapinduzi Party, which fielded Magufuli, 56, a minister for public works. REUTERS/Sadi Said – RTX1TYDQ

    Rais Dkt JP Magufuli amekataa ombi la Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi, aliyeomba kustaafu kuwa Mdhamini wa Skauti Tanzania.
    Rais Dkt Magufuli amesema, bado vijana wana mambo mengi ya kujifunza kutoka kwake.

  • Dkt. Arnold Kihaule ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

    Dkt. Arnold Kihaule ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Arnold Mathias Kihaule kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

    Uteuzi wa Dkt. Kihaule unaanza leo tarehe 03 Oktoba, 2018.

    Kabla ya uteuzi huo Dkt. Kihaule alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU)

  • Dar es Salaam; Salama zaidi kwa wanawake afrika mashariki

    Dar es Salaam; Salama zaidi kwa wanawake afrika mashariki


    Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania ndilo jiji ambalo wasichana na wanawake wanajihisi wakiwa salama zaidi miongoni mwa miji mikuu ya kibiashara Afrika Mashariki.

    Hii ni kwa mujibu wa ripoti kuhusu usalama wa wanawake na wasichana dhidi ya udhalilishaji katika miji mbalimbali duniani uliofanywa na shirika la Plan International.
    Jiji la Kampala linaongoza kwa kuwa hatari zaidi, ambapo wataalamu wanasema wasichana na vijana wa kike wamo katika hatari ya juu zaidi ya kudhalilishwa wa kingono wakiwa katika maeneo ya umma.
    Sharon, mama mwenye miaka 19 anayeishi mtaa wa mabanda Kampala, aliambia Plan International kwamba matokeo hayo si ya kushangaza hata kidogo.

    Utafiti huo uliangazia miji 22 na kuwahusisha wataalamu wa masuala ya haki za watoto na wanawake karibu 400 katika miji hiyo.
    Wataalamu walikadiria hatari kwa kueleza miji waliyohisi ina hatari ya juu na hatari ya juu zaidi.

    Katika miji ya Bogota na Johannesburg, kulikuwa na maafikiano kwamba si salama hata kidogo.
    Kwa jumla, mji wa tatu duniani kwa kutokuwa salama kwa wanawake ni Delhi kisha inafuata Lima kabla ya kufikia Kampala.
    Mji wa Kampala hata hivyo unaongoza kwa kuwa na kiwango cha juu cha ‘hatari kuwa juu zaidi’.

    Jiji kuu la Kenya, Nairobi linaifuata Kampala ingawa kwa kiwango chake cha ‘hatari kuwa juu zaidi’ ni chini ya asilimia 40.
    Baada ya Nairobi, kuna Cairo, Sao Paulo, Dhaka, Jakarta na Paris kabla ya kuifikia Dar es Salaam ambao ni mji wa 12 kwenye orodha ya jumla.

    Kwa kuangazia unyanyasaji wa kingono na ubakaji, Johannesburg inaongoza ikifuatwa na Kampala, huku Nairobi ikiwa ya nne na Dar es Salaam ya 13.
    Mmoja wa waliochangia kutoka Johannesburg alisema: “Unyanyasaji wa kingono hutokea mara nyingi sana kiasi kwamba tunahisi ni jambo tunalofaa kutafuta njia za kulizoea kuishi nalo na kuendelea na shughuli zetu.”
    Kwa wizi na uchopozi, Johannesburg inaongoza, Kampala ni ya nne ikifuatwa na Nairobi. Dar es Salaam inapanda juu kidogo ikilinganishwa na visa vingine, ambapo hapa inashikilia nafasi ya 10.

  • RAIS MAGUFULI KUZINDUA FLYOVER YA TAZARA KESHO

    RAIS MAGUFULI KUZINDUA FLYOVER YA TAZARA KESHO

    RAIS Dkt. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Daraja la Juu ‘flyover’ mpya iliyojesgwa hivi karibuni katika makutano ya Barabara za Mandela na Nyerere katika eneo la TAZARA jijini Dar es Salaam.

    Tukio hilo litafanyika kesho Alhamisi, kesho Septemba 27, 2018 ambapo Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda amesema Flyover hiyo itapunguza changamoto ya msongamano barabarani iliyokuwa inaleta hasara ya Tsh. Bilioni 400 kwa mwezi.

    Makonda amewaalika viongozi wa upinzani kwenda kushuhudia tukio hilo na kuwa atawawekea sehemu maalumu ya kukaa akiamini wao ndio wanaongoza kuponda maendeleo hayo na kwamba Flyover hiyo ilianza kutumika kwa majaribio mnamo Septemba 15 mwaka huu.

  • Damas Daniel Ndumbaro Ateuliwa Kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani

    Damas Daniel Ndumbaro Ateuliwa Kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani

    Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akichukua nafasi ya Susan Kolimba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

    Aidha, Magufuli amemteua Dkt Faraji Mnyepe kuwa Katibu Mkuu Wizara hiyo ya Mambo ya Nje akichukua nafasi ya Prof Adolf Mkenda.

  • TEF watuma salamu za rambirambi, yataka elimu ya majanga iongezwe

    TEF watuma salamu za rambirambi, yataka elimu ya majanga iongezwe

     

    Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limetoa salamu za pole kwa Rais John Magufuli, familia, ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao katika ajali ya Kivuko cha MV Nyerere.

    Salamu hizo zimetolewa Jana Septemba 23,2018 na Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deodatus Balile ambaye amesema wamepokea kwa mshituko taarifa za kupinduka kwa kivuko hicho.

    Amesema ajali hiyo inarejesha kumbukumbu mbaya kwa Watanzania kwani inawakumbusha ajali za MV Bukoba iliyotolea Mei 21 mwaka 1996 katika Ziwa Victoria ambako watu zaidi ya 800 walipoteza maisha.

    Amesema MV Spice Islander mwaka 2011 katika Bahari ya Hindi, ambako zaidi ya watu 200,walipoteza maisha, huku MV Skagit nayo ikizama kwenye bahari hiyo hiyo nakupoteza maisha ya watu karibu 150 mwaka 2012.

    “TEF inatoa pole kwa Rais, familia za wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki. Tunafikiri wakati umefika wa Tanzania kuzuia kuendelea kushuhudia majanga kama haya ambayo kwa hakika yanataka kugeuka kuwa utamaduni wa uendeshaji wa vyombo vya majini nchini,” amesema.

    “Tunaisihi Serikali, wananchi na wadau mbalimbali kuongeza elimu ya udhibiti na tunaisihi Serikali, wananchi na wadau mbalimbali kuongeza elimu ya udhibiti wa majanga, huku tukijenga utamaduni wa kuheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kwa usalama wa abiria,” amesema Balile.

    Balile amesema wana imani utafanyika uchunguzi wa kina na waliohusika na uzembe huu uliogharimu maisha ya Watanzania watafikishwa katika vyombo vya sheria.

    “Tunaomba katika kipindi hiki kigumu tuwe na utulivu, tuendeleze umoja na mshikamano wa Watanzania, huku tukivisihi vyombo vya dola vinavyofanya uchunguzi kuharakisha uchunguzi na kuwatendea haki waliohusika kwa mujibu wa sheria,” amesema.

    Balile amesema, “Tunaomba Mungu awape nafuu manusura waliojeruhiwa na pumziko la milele Watanzania wenzetu waliopoteza maisha. Amina.”

  • Updete Ajali ya Mv Nyerere Mwanza

    Updete Ajali ya Mv Nyerere Mwanza

    RC wa Mwanza, John Mongela amesema idadi ya watu waliofariki kwa ajli ya kuzama Ziwa Victoria imeongezeka na kufikia 94 leo asubuhi. DC Ukerewe amesema Kivuko kilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 100 na tani 25 za mizigo, lakini kibeba abiria zaidi ya 400.

     

    Vikosi vya uokoaji mkoa wa Mwanza vimeongezewa nguvu na vikosi vya mkoa wa Mara katika eneo la tukio kuongeza kasi ya kuokoa na kuopoa watu waliopinduka na kivuko hicho. Mkuu wa Jeshi la polisi IGP Simon Sirro na Waziri wa Uchukuzi Isaac Kamwelwe wamefika eneo la tukio kushiriki uokoaji.

     

    Wakati uokoaji na uopoaji ukiendele mamia ya wakazi wa visiwa hivyo wamefurika kituo cha afya cha Bwisya kutambua jamaa zao walioopolewa. Tayari uongozi wa wakala wa meli mkoa wa Mwanza umetambua wafanyakazi wa kivuko watano ambao wamepoteza maisha akiwemo   nahodha, fundi, Karani, mlinzi na mkuu wa kivuko, Kivuko hicho kilikuwa na wafanyakazi wanane.

  • SIMBA YAWEKA REKODI NYINGINE

    SIMBA YAWEKA REKODI NYINGINE

    Klabu ya Simba imeendelea kuweka rekodi kwa msimu wa pili mfululizo kuwa ni timu ya kwanza kwa kutoa mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu Bara.

    Msimu huu mshambuliaji Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda Meddie Kagere ndiye alikuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti msimu huu baada ya kucheza michezo mwili.

    Msimu wa uliopita Simba ndiyo ilifungulia kwa kutoa mchezaji bora wa mwezi ambaye alikuwa ni Mganda Emmanuel Okwi alikuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti 2017 huku akiweka na rekodi ya kuweka ya ‘hat trick’ ya kwanza ligi kuu.

    Hata hivyo msimu wa mwaka 2016/17 mchezaji bora wa mwezi wa kwanza alikuwa ni John Bocco ambaye alikuwa Azam FC na sasa anakipiga katika klabu ya Simba na msimu uliopita alikuwa mchezaji bora wa mwezi Januari.

  • Miili 44 ya waliofariki katika Kivuko inavyotolewa majini

    Miili 44 ya waliofariki katika Kivuko inavyotolewa majini

    Zoezi la uokoaji wa abiria waliokuwemo katika kivuko cha MV Nyerere kilichozama limesitishwa kutokana na giza na litaendelea leo alfajiri ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela amesema mpaka sasa watu waliyookolewa wakiwa hai ni 37 na waliopoteza maisha ni 44.

    RC Mongela amesema Kivuko hicho haikujulikana kilikuwa na idadi ya watu wangapi.