CHAWATA SERIKALI KUSIMAMIA SHERIA NA KANUNI ZA USALAMA BARABARANI

CHAWATA SERIKALI KUSIMAMIA SHERIA NA KANUNI ZA USALAMA BARABARANI

Like
364
0
Tuesday, 24 May 2016
Local News

CHAMA cha Walemavu Tanzania-CHAWATA-kimeitaka Serikali kupitia kikosi cha usalama barabarani kusimamia sheria na kanuni za usalama barabarani ili kunusuru vijana wanaopata ulemavu kupitia ajali zinazotokana na usafiri wa bodaboda.

 

Akizungumza na EFM Mweyekiti wa CHAWATA John Mlabu amesema tangu kuanza kwa biashara ya usafiri wa bodaboda Nchini kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wenye ulemavu ambao baadae wanakuwa tegemezi kwa Taifa badala ya kuwa ni wazalishaji.

 

Aidha amewataka madereva wa magari pamoja na wa bodaboda kufuata sheria za usalama barabarani ili kunusuru maisha ya watu pamoja na kupunguza ongezeko la watu wanaopata ulemavu kila siku kutokana na ajali za barabarani.

Comments are closed.