DARESALAAM INATARAJIWA KUWA NA WATU MILIONI 10 IFIKAPO 2030

DARESALAAM INATARAJIWA KUWA NA WATU MILIONI 10 IFIKAPO 2030

Like
240
0
Thursday, 05 May 2016
Local News

MKOA wa Dar es salaam unatarajiwa kuwa na watu milioni 10 ifikapo mwaka 2030 hivyo ni muhimu kuzingatia uboreshaji wa Jiji kulingana na idadi ya watu.

 

Hayo yamebainishwa leo na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake ambapo amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa ongezeko la watu serikali ilibuni mradi wa uendelezaji wa Jiji kwa ufadhili wa benki ya dunia.

 

Amesema kuwa ukuaji wa Jiji la Dar es salaam unakabiliwa na makazi yasiyopimwa kwa asilimia 70 hadi 80 hivyo kutokana na ukuaji huo na mabadiliko ya Tabia nchi athari kama vile mafuriko zinatarajia kuongezeka Jijini Dar es salaam.

Comments are closed.