DOLA 150000 ZATOLEWA KATIKA KIJIJI CHA MACHALI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

DOLA 150000 ZATOLEWA KATIKA KIJIJI CHA MACHALI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

Like
273
0
Tuesday, 24 November 2015
Local News

KIJIJI cha Manchali kilichopo wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, kimekabidhiwa mradi wenye thamani ya dola za Marekani 150,000 kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

 

Akikabidhi mradi huo Mratibu wa mashirika ya Umoja wa mataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Alvaro Rodriguez amesema mradi huo umelenga kuisaidia jamii inayoishi katika kijiji hicho kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha zinazotokana na mabadiliko hayo.

 

Mradi huo pia umelenga kutatua tatizo la nishati na kufanya matumizi bora ya ardhi na teknolojia ya maji ambapo jumla ya familia 600 zitanufaika na mradi husika.

Comments are closed.