NIGERIA: BUHARI AAGIZA KUKAMATWA KWA AFISA ANAETUHUMIWA KWA WIZI

NIGERIA: BUHARI AAGIZA KUKAMATWA KWA AFISA ANAETUHUMIWA KWA WIZI

Like
198
0
Wednesday, 18 November 2015
Global News

RAIS wa Nigeria Muhammadu Buhari ameagiza kukamatwa kwa Afisa mmoja mkuu serikalini kwa tuhuma za kuiba zaidi ya dola bilioni 2 zilizotengwa kwaajili ya vita dhidi ya kundi la Boko Haram.
Kanali Sambo Dasuki ambaye alikuwa mshauri wa kitaifa kuhusu masuala ya usalama kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan, ameshtakiwa kwa kutoa kandarasi bandia za kununua helikopta 12, ndege 4 za kijeshi na silaha mbalimbali.
Msemaji wa rais Buhari amesema kwamba ufisadi huo ulisababisha vifo vya maelfu ya raia wa Nigeria.ingawa mshauri huyo wa zamani anayedaiwa kuiba fedha hizo amekana madai hayo.

Comments are closed.