TFDA YAKUTANA NA WADAU WA USALAMA WA CHAKULA

TFDA YAKUTANA NA WADAU WA USALAMA WA CHAKULA

Like
256
0
Monday, 16 May 2016
Local News

MAMLAKA ya chakula na dawa-TFDA  imekutana na adau mbalimbali wa usalama wa chakula na dawa kutoka nchi 12 za bara la Africa ikiwemo Tanzania kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kiutendaji kazi utakaochangia kutatua changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo.

 

Akizungumza jijin dar es salaam, Mkurugenzi mkuu wa TFDA HIIT SILLO amesema kuwa kupitia mkutano huo wadau wataweza kuchambua ubora wa maabara zinazozingatia viwango vya upimaji vya vakula, dawa pamoja na viwango vya uchunguzi wa vyakula.

 

Hata hivyo sillo ametoa rai kwa wafanyabiashara nchini wanaopitisha bidhaa zao kutoka nje bila kufuata kanuni na taratibu za mamlaka ya chakula na dawa kuacha mara moja kwani hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao .

Comments are closed.