WHO YATOA MASHAKA UENEAJI WA ZIKA

WHO YATOA MASHAKA UENEAJI WA ZIKA

Like
202
0
Wednesday, 15 June 2016
Global News

Kamati ya dharura ya shirika la afya duniani imetoa tathmini kuwa kuna uwezekano mdogo kidogo cha maambukizi ya virusi ZIKA kuenea katika mataifa mengine ,hivyo mashindano ya Olympic hayana haja ya kuhamishwa nchini Brazil.Ingawa tayari kulikuwa na wito wa michuano hiyo ya Rio kuahirishwa au kuhamisha mashindano hayo.

Shirika la afya ulimwenguni WHO, kwa mara nyingine limetoa angalizo la awali kukataza watu kutosafiri au kufanya biashara katika maeneo ambayo kwa sasa yana virusi vyua ZIKA.

Hata hivyo shirika hilo limewataka wanawake wajawazito kujizuia kwenda kushuhudia michuano hiyo na kuwa waangalifu kuumwa na mbu ambao wanasambaza virusi vya ZIKA.

Dr. Bruce Aylward ni mkuu wa shirika la afya dunia kitengo cha magonjwa ya mlipuko na dharura

”Kamati imethibitisha kuwa kuna uwezekano mdogo wa virusi hivyo kuenea katika mataifa mengine wakati wa mashindano ya Olympic.

Wakati huo pia itakuwa ni majira baridi,kiasi kwamba ni vigumu kuenea kwa virusi hivyo nchini Brazil kwa kuwa msimu huo unajumuisha mwezi august na septemba . Jambo jingine ni kwamba kamati hiyo imeweza kuangalia kiini cha tatizo na kutafuta njia za kukabiliana na matatizo yaliyopo nchini Brazil na kujua namna watakavyochangia kuondoa maambukizi.”

Kati ya mwezi Februari na Aprili mwaka huu Brazil ilibaini jumla ya watu 90,000 wakiwa na maambukizi ya virusi hivyo.

Comments are closed.