11 WAFARIKI KWA KUKANYAGANA ZIMBABWE

11 WAFARIKI KWA KUKANYAGANA ZIMBABWE

Like
348
0
Friday, 21 November 2014
Global News

WATU 11 wamefariki katika mkanyagano nchini Zimbabwe baada ya ibada ya kidini kufanyika katika uwanja wa soka.

Polisi wanasema kuwa watu wanne wamefariki katika uwanja huo ulio mjini Kwekwe wakati wengine saba wakifariki hospitalini.

Mkanyagano huo ulitokea wakati maelfu ya waumini wakikimbilia kuondoka uwanjani humo baada ya ibada iliyoongozwa na mhubiri wa kipentekoste Walter Magaya kumalizika.

Comments are closed.