JUMLA ya watu 11 wameuawa kufuatia shambulio lililotokea kaskazini mashariki mwa Kenya ambapo inahofiwa kuwa shambulio hilo lilikuwa na nia ya kuwalenga wafanyikazi wa machimbo ya mawe wasiokuwa wenyeji wa eneo hilo.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa kuwa ilisikika sauti kubwa ya milipuko miwili kisha ikafuatiwa na milio ya risasi huku Shirika la msalaba mwekundu tayari limeshaanza jitihada za kuwaokoa majeruhi ambao idadi kamili haijulikani.
Hata hivyo haijathibitishwa wahusika wa shambulio hilo ingawa kwa kipindi kirefu wanamgambo wa kundi la Al shabaab wamekuwa wakilenga wakazi wasio wenyeji wa asili katika eneo hilo.
Picha juu ni sehemu ya tukio katika kijiji cha Soko Mbuzi