121 MBARONI KWA MAKOSA YA KIHALIFU

121 MBARONI KWA MAKOSA YA KIHALIFU

Like
276
0
Thursday, 01 October 2015
Local News

JESHI la polisi nchini kwa kushirikiana na ofisi za interpol kanda ya kusini mwa afrika limefanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 121 kwa makosa mbalimbali ya kihalifu baada ya kufanya operesheni ya pamoja kutokana na maamuzi yaliyoafikiwa kwenye mikutano ya wakuu wa majeshi wa nchi za kusini mwa Africa-SARPCCO.

Akizungumza leo jijini dar es salaam, Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai CP Diwani Athumani amesema kuwa watuhumiwa wamekutwa na vielelezo vya uhalifu zikiwemo nyara za serikali, dawa za kulevya , madini pamoja na bidhaa na dawa zilizopigwa marufuku.

Comments are closed.