129 WAFARIKI DUNIA BAADA YA KIVUKO KUZAMA CONGO

129 WAFARIKI DUNIA BAADA YA KIVUKO KUZAMA CONGO

Like
323
0
Monday, 15 December 2014
Global News

MIILI ya watu wapatao 129 imepatikana kutoka Ziwa Tanganyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, baada ya feri kupinduka na kuzama mapema siku ya Ijumaa.

Waziri wa Uchukuzi nchini humo Laurent Sumba Kahozi amesema bado zoezi la kuwatafuta watu waliopotea katika ajali hiyo linaendelea.

Maafisa katika jimbo la Katanga wamesema upepo mkali na kujaza abiria na mizigo kupita kiasi kumesababisha boti ya MV Mutambala, kupinduka.Wanawake na watoto ni miongoni mwa watu waliokumbwa na ajali hiyo ambayo ilitokea mapema Ijumaa asubuhi.

 

 

Comments are closed.