13,491 WAGUNDULIKA KUWA NA KIPINDUPINDU

13,491 WAGUNDULIKA KUWA NA KIPINDUPINDU

Like
268
0
Monday, 11 January 2016
Local News

JUMLA ya Watu elfu 13,491 wamegundulika kuwa na ugonjwa wa Kipindupindu tokea kuanza kwa ugonjwa huo Agosti 15 Mwaka jana na kuwa kati yao jumla ya watu 205 wameshafariki kwa ugonjwa huo.

 

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ahmis Kigwangala, wiki iliyoaanza tarehe 4 hadi leo 11 Januari,  kumekuwa na jumla ya Wagonjwa 615 walioripotiwa nchini na vifo 3 hali inayoonyesha kuwa hali ya kipindupindu nchini bado sio nzuri.

 

Comments are closed.