TAKRIBAN watu 140 wameuawa kwa milipuko ya mabomu katika miji ya Homs na Damascus nchini Syria, waangalizi na vyombo vya habari vya serikali wameeleza.
Inaelezwa kuwa milipuko minne ilitokea katika eneo la Sayyida Zeinab mjini Damascus na kuua takriban watu 83, ambapo awali mjini Homs Watu 57 wengi wao raia waliuawa kwa mashambulizi ya mabomu yaliyokuwa yametegwa kwenye magari mawili.
Wanamgambo wa Islamic State wamekiri kutekeleza mashambulizi hayo katika miji hiyo yote miwili.