16 WATIWA NGUVUNI BRUSSELS

16 WATIWA NGUVUNI BRUSSELS

Like
254
0
Monday, 23 November 2015
Global News

UBELGIJI imesema kuwa imewakamata watu 16 katika operesheni ya polisi ya kupambana na ugaidi mjini Brussels.

Katika msako huo, nyumba kumi na tisa zimekaguliwa, ingawa hakuna silaha zilizokamatwa. huku mtuhumiwa mkuu wa shambulio lililotokea mjini Paris, Salah Abdeslam, bado hajakamatwa.

Operesheni hiyo ya polisi kuhusiana na tishio la ugaidi mjini Brussels imemalizika bila kupatikana kwa vithibitisho vya kutosha kwa wahusika hali iliyosababisha mamlaka ya mji huo kuongeza muda ili kufanya uchunguzi Zaidi wa tukio hilo.

Comments are closed.