LIVERPOOL YAMTIMUA BRENDAN RODGERS

LIVERPOOL YAMTIMUA BRENDAN RODGERS

Like
290
0
Monday, 05 October 2015
Slider

Klabu ya soka ya Uingereza Liverpool imemtimua meneja wake Brendan Rodgers siku ya jana baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitatu na nusu.

Baada ya maamuzi hayo kufanyika aliyekuwa bosi wa klabu ya Borussia Dortmund, Jurgen Klopp anatazamwa kuwa chaguo la kwanza kuchukua nafasi ya Brendan Rodgers

Maamuzi ya kumtimua Rodgers yalifikiwa siku ya jumapili kabla ya kutoka sare ya 1-1 kwenye mchezo wao dhidi ya Everton

Uongozi wa klabu hiyo katika maelezo waliyoyatoa wanaamini hayo ni miongoni mwa maamuzi magumu kuwahi kufikiwa na klabu hiyo lakini wanaamini wananafasi ya kufanikiwa

 

MAJINA YA WANAOTAZAMIWA KUCHUKUA NAFASI YA BRENDAN RODGERS

Jurgen Klopp: aliyekuwa meneja wa Borussia Dortmund
Carlo Ancelotti: aliyekuwa meneja wa Real Madrid, Chelsea na PSG
Frank de Boer: meneja wa Ajax
Walter Mazzarri: aliyewahi kuwa meneja wa Inter Milan
Jurgen Klinsmann: meneja wa United States

Comments are closed.