20 WAFARIKI, LIGI KUU YASIMAMISHWA MISRI

20 WAFARIKI, LIGI KUU YASIMAMISHWA MISRI

Like
567
0
Monday, 09 February 2015
Global News

MISRI  imesimamisha kwa muda usiojulikana ligi kuu ya nchi hiyo baada ya watu zaidi ya  20 kufariki dunia.

Kati ya waliofariki wengi wao ni Mashabiki wa timu ya Zamalek ambao walifariki kutokana na msongamano wakati Polisi walipowafyatulia mabomu ya machozi baadhi ya mashabiki waliokuwa wakijaribu kuingia kwa nguvu ndani ya uwanja wakati timu hiyo ilipokuwa ikipambana na timu ya ENPPI. (INI-P)

Taarifa ya Wizara ya mambo ya ndani ya Misri inasema kuwa Mashabiki wa Zamalek walikuwa wanataka kuingia uwanjani kwa nguvu hivyo walikuwa wakiwazuia ili kunusuru mali ya uma isiharibike.

_80872653_025785065-2 _80872596_025784902-2 _80872293_80872292 _80870709_80870708 _80872661_025784356-2

 

 

Comments are closed.