26 WAUAWA MISRI

26 WAUAWA MISRI

Like
257
0
Friday, 30 January 2015
Global News

MAAFISA wa Jeshi nchini Misri wamesema takriban watu 26 wameuawa katika mfululizo wa mashambulizi yaliyofanywa na kundi la wapiganaji la Islamic State Kaskazini mwa Misri katika eneo la Sinai

Wamesema gari lililokuwa na mabomu lilipiga kituo cha kijeshi kaskazini mwa Sinai katika mji wa El-Arish yakilenga hoteli ya jeshi na kuwaua wanajeshi kadhaa. Mashambulizi mengine kama hayo yalifanyika katika mji jirani wa Sheik Zuwayid na mji wa Rafah katika mpaka wa Gaza.

Wakati huo huo kundi la wapiganaji la Ansar Beit al-Maqdis ambalo ni mshirika wa wapiganaji wa Islamic State wamekiri kutekeleza shambulio hilo.

Comments are closed.