Mtoto wa kike ambaye ilithibitishwa kuwa ana Ebola akiwa na siku sita pekee amepona, maafisa afya huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wamethibitisha.
Mama yake na mtoto Benedicte alikuwa ameambukizwa ugonjwa wa Ebola na alifariki wakati anajifungua.
Benedicte alianza kuonesha dalili siku chache baada ya kuzaliwa na madaktari walikuwa na wiki tano tu kumtibia na kuhakikisha anakuwa hai
Baba na shangazi yake walimpeleka nyumbani siku ya Jumatano wiki iliyopita.
“Baba yake, Thomas, alikuwa na hisia kali… ndio mtoto wangu wa kwanza,” msemaji wa wizara ya afya ameiambia BBC.
Ebola ni ugonjwa hatari hupelekea kifo haraka na huambatana na homa kali, kutapika, kuharisha, na kutoka damu nje na ndani.
Nusu ya wanao ambukizwa hufariki, lakini watoto ni ngumu sana kupona.
Tangu ugonjwa huo ulipo lipuka tena sasa hivi kuna taarifa za kesi 27 za ugonjwa huo kwa watoto ambao walikuwa bado hawajafikisha mwaka mmoja na 21 walifariki.
Taarifa kama za kupona kwa Benedicte ni adimu sana.
Alizaliwa tarehe 31 Octoba 2018 na alikuwa akitibiwa katika kituo cha Ebola huko Beni, mji uliotandikwa sana na mlipuko wa ugonjwa huo DRC.
Benedicte ndiye mgonjwa mdogo zaidi ambae madakrari na watu wanao jitolea wamemhudumia.
Mtoto huyo wakike sasa anajulikana kama “muujiza wa Beni”