40 WAFA KUTOKANA NA MLIPUKO WA MABOMU NIGERIA

40 WAFA KUTOKANA NA MLIPUKO WA MABOMU NIGERIA

Like
505
0
Friday, 12 December 2014
Global News

MABOMU mawili yameripuka katika mji wa Jos nchini Nigeria, hilo likiwa ni shambulizi la pili kuukumba mji huo na kuwaua watu 40 huku wengine wakijeruhiwa.

Taarifa zimeeleza kuwa hakuna kundi ambalo limekiri kuhusika na mashambulizi hayo lakini inashukiwa ni waasi wa kundi la Boko Haram wamefanya mashambulizi hayo.

Mnamo mwezi Mei mwaka huu Boko Haram iliushambulia mji huo wa Jos ulioko kati mwa Nigeria na kuwaua watu 118.

                                                                                            

Comments are closed.