6 WATHIBITISHWA KUUGUA KIPINDUPINDU ARUSHA

6 WATHIBITISHWA KUUGUA KIPINDUPINDU ARUSHA

Like
446
0
Thursday, 29 October 2015
Local News

JUMLA ya watu 27 walioripotiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa kipindupindu Jijini Arusha kati yao 6 wamethibitishwa kuwa na ugonjwa huo ambapo hadi sasa watano wamelazwa katika kituo cha Afya cha Levolosi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkurlu amewataka wakazi wa Jiji la Arusha kufuata kanuni Afya ili kuepuka ugonjwa.

Nkurlu amesema kuwa kwa zaidi ya miezi miwili sasa maeneo mbali mbali nchini yameripotiwa kuwa na ugonjwa huo ikiwemo mikoa ya Dar es salaam, Morogoro na Pwani.

Comments are closed.