7 WAPOTEZA MAISHA BAADA YA WATU WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI KUVAMIA KITUO CHA POLISI CHA STAKISHARI

7 WAPOTEZA MAISHA BAADA YA WATU WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI KUVAMIA KITUO CHA POLISI CHA STAKISHARI

Like
443
0
Monday, 13 July 2015
Local News

JUMLA ya watu saba wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi ambao wamevamia kituo cha polisi cha Stakishari usiku wa kuamkia leo kilichopo ukonga jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini –IGP-ERNEST MANGU amesema kuwa miongoni mwa watu waliouawa ni Askari 4 na raia 3 ambapo kati ya raia hao watatu waliouawa mmojawapo ni jambazi.

IGP Mangu amebainisha kwamba watu wengine watatu waliokuwa katika eneo hilo pamoja na Askari mmoja wamejeruhiwa na wamepelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya matibabu ambapo ameeleza kuwa lengo la majambazi hao ilikuwa ni kupora silaha katika kituo hicho.

Comments are closed.