70 WAUAWA KWA MABOMU SYRIA

70 WAUAWA KWA MABOMU SYRIA

Like
404
0
Monday, 01 February 2016
Global News

WATU zaidi ya  70 wameuawa kutokana na mashambulio  ya mabomu ambayo kundi la magaidi wanaoitwa Dola  la  Kiislamu limedai kuyafanya karibu  na sehemu takatifu ya Washia nje ya mji mkuu wa Syria, Damascus.

 

Kwa mujibu  wa  taarifa  iliyotolewa  na kituo kilichopo mjini London, kinachofuatilia haki za binadamu nchini  Syria, watu  hao waliuawa kutokana  na miripuko miwili ya mabomu karibu na  sehemu hiyo takatifu, Sayyida Zeinab.

 

Watoto kadhaa walikuwamo miongoni mwa walioangamizwa huku Watu wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa.

Comments are closed.