90 WATEKWA NYARA NA IS SYRIA

90 WATEKWA NYARA NA IS SYRIA

Like
407
0
Tuesday, 24 February 2015
Global News

KUNDI la Islamic State limewateka nyara watu 90 wa jamii ya wakristo kutoka katika kijiji kimoja kazkazini mwa Syria.

Tukio hilo la utekaji nyara limefanyika mapema leo alfajiri, baada ya wanamgambo hao kuchukua udhibiti wa vijiji kadhaa kutoka kwa walinda usalama wa kabila la Wakurdi.

Wanamgambo hao walivamia kituo cha Radio na kuchukua udhibiti wa mawasiliano na kuanza kutangaza Radioni, kuwa wamewateka nyara wale wanaojiita watetezi wa Dini.

Comments are closed.