DONDOO ZA TENNIS- PARIS MASTERS

DONDOO ZA TENNIS- PARIS MASTERS

Like
395
0
Wednesday, 29 October 2014
Slider

Bingwa nambari moja duniani katika mchezo wa Tennis, Novak Djokovic amefanikiwa kutinga katika hatua ya raundi ya pili baada ya kumchapa Mjerumani, Phillip Kohlschreiber kwa seti 6-3 6-4.

Djokovic mwenye umri wa miaka 27, alionekana akiwa katika kiwango kizuri dhidi ya Phillip huku akipambana kutopoteza taji la ubingwa nambari moja dhidi ya Mswisi Roger Federer.

Federer anayetarajiwa kushuka leo uwanjani dhidi ya Mfaransa Jeremy Chardy anaalama 9,280 nyuma ya Djokovic mwenye jumla ya alama 11,510 kuelekea katika michuano ya ATP World Tours Finals huko O2 Arena, London.

Ushindi huo wa Mserbia Djokovic umekuja wiki moja tu baada ya mke wake kujifungua mtoto wa kiume waliyempa jina la Stefan.

novak-djokovic-training

Novak Djokovic

djokovic-training

novak-djokovic-sharapova-training

Comments are closed.