RAIS WA ZAMBIA MICHAEL SATTA AMEFARIKI DUNIA HUKO LONDON

RAIS WA ZAMBIA MICHAEL SATTA AMEFARIKI DUNIA HUKO LONDON

Like
705
0
Wednesday, 29 October 2014
Local News

RAIS wa Zambia Michal Satta amefariki akiwa London, Uingereza ambako alikuwa akitibiwa ugonjwa ambao bado haujawekwa wazi.

Huyu ni Rais wa Pili wa nchi hiyo kufariki akiwa madarakani baada ya Rais Levy Mwanawasa naye kufariki dunia akiwa madarakani miaka kadhaa iliyopita.

Kulikuwa na uvumi kuwa Sata alikuwa mgonjwa sana na hajaonekana hadharani tangu aliporejea kutoka katika mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York mwezi uliopita, ambako alishindwa kutoa hotuba aliyopangiwa kuitoa.

Alisafiri kwa njia ya ndege kwenda London wiki moja iliyopita kwa ajili ya matibabu.

Michael Chilufya Sata alizaliwa mwaka 1937 katika mji wa Mpika, eneo ambalo lilikuwa wakati huo ni Northern Rhodesia. Muumini wa dini ya Kikristo ya madhehebu ya Katoliki, alifanya kazi kama afisa polisi, mfanyakazi wa reli na mwanachama wa chama cha wafanyakazi wakati wa utawala wa kikoloni. Baada ya Zambia kupata uhuru wake, pia aliishi kipindi fulani mjini London, akiwa mfanyakazi wa reli, na kurejea Zambia, akiwa na kampuni ya teksi.

 

 

 

Comments are closed.