Msanii kutoka marekani mzaliwa wa Saint Michael, huko Barbados, mwaka 1988 February 20, alifungiwa kuendelea kutumia mtandao wa instagram kwa takribani miezi sita mara baada ya kukiuka taratibu za mtandao huo.
miezi michache nyuma msanii huyo alipost picha yake kwenye akaunti ya Instagram akiwa hana top kuziba mwili wake sehem ya juu hivyo kumfanya kuwa mtupu picha alizopiga kwenye photoshoot ya jarida la Lui.
picha hiyo iliondolewa haraka na uongozi wa mtandao huo na akaunti yake ilifutwa kabisa baada ya muda mfupi lakini timu ya wataalamu wa mtandao huo walidai ilifutika kwa bahati mbaya na hivyo baadae waliirudisha tena.
Rihana hakuwahi kusema lolote kuhusiana na tukio hilo na badala yake aliacha kabisa kutumia mtandao huo
msanii huyo mwenye followers milion 12 amepokelewa kwa kishindo na mashabiki wake pamoja na mtandao wenyewe wa instagram
wasemaji wa mambo wanaamini kwamba huenda mtandao huo pia umemrudisha kwa kutambua ushawishi wake mkubwa alionao kwenye mtandao huo.