VIONGOZI wa vyama vya ushirika wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi wameiomba wizara ya kilimo na ushirika kutoa elimu kwa wanachama juu ya sheria mpya ya ushirika ili iweze kutambulika na upunguza migogoro na mivutano inayosababisha vyama kugawanyika na kukosa nguvu ya kiuchumi na uzalishaji.
Ombi hilo limetolewa na viongozi wa vyama vya ushirika vya MAKINI , MKOTOKUYANA,NDOMONI na MARAMBO wakati walipokuwa wanazungumza na waandishi wa habari wilayani humo.
MOHAMEDI MUSA mwenyekiti wa chama cha msingi Makini amesema pamoja na serikali kuleta sheria mpya ya ushirika lakini viongozi na wanachama wa vyama hivyo hawajaziona sheria na serikali haina budi kutoa elimu kwa wanaushirika ili waweze kuzitambua.
Amesema kuwa kuwepo kwa sheria hizo mpya kumevifanya vyama vya ushirika kugawanyika na kusababisha mapato ya vyama kuwa madogo jambo ambalo linatishia uhai na kuwa nauwezekano wa kufa kwa vyama hivyo kutokana na kuwa na uzalishaji mdogo.