DAKTARI MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA SIERRA LEONE

DAKTARI MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA SIERRA LEONE

Like
314
0
Tuesday, 04 November 2014
Global News

DAKTARI mwingine amekufa kwa ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone.

Daktari huyo ambaye alikuwa muuguzi mkuu katika hospitali ya Kambi kaskazini mwa Siearra Leone ni wa tano kuuawa na ugonjwa huo nchini humo na inaaminika kwamba aliambukizwa Ebola na mgonjwa ambaye alimtibu maradhi mengine, kwa sababu hakuwahi kumtibu mgonjwa mwenye maradhi hayo hatari.

Kwa ujumla, wahudumu wa afya wapatao 100 wameuawa na maradhi hayo nchini Sierra Leone. Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limesema watu zaidi ya 4,900 wamekufa kutokana na Ebola katika mataifa ya Afrika Magharibi, na wapatao 13,000 wameambukizwa ugonjwa huo.

 

Comments are closed.