BARAZA LA MITIHANI LIMEIDHINISHA KUTOA MATOKEO YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI

BARAZA LA MITIHANI LIMEIDHINISHA KUTOA MATOKEO YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI

Like
374
0
Wednesday, 05 November 2014
Local News

BARAZA la Mitihani la Tanzania limeidhinisha kutoa matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya msingi uliuofanyika September 10 hadi 11mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Katibu mtendaji wa Baraza la mitihani Dokta CHARLES MSONDE ameeleza kuwa jumla ya watahiniwa 808,085 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 429,624 sawa na asilimia 53.17 na wavulana 378,461 sawa na asilimia 46.83.

Dokta MSONGE amethibitisha kuwa jumla ya watahiniwa 451,392 kati ya watahiniwa 792,118 waliofanya mtihani huo wamepata alama 100 ya ufaulu kati ya alama 250 ikiwa ni asilimia 56.99.

Comments are closed.