MATOKEO ya awali ya uchaguzi mdogo nchini Marekani yanaonesha kuwa chama cha Republican kimechukua udhibiti wa baraza la Seneti kwa kupata kiasi ya viti 51 katika baraza hilo lenye viti 100.
Pia chama hicho kinaelekea kupata ushindi wa kishindo katika baraza la wawakilishi kwa miongo kadhaa. Warepublican wamefaidika na wimbi la kutoridhika kwa wapiga kura na kutoa pigo kwa rais Barack Obama ambalo litapunguza uwezo wake wa kupitisha ajenda zake katika bunge.
Hata hivyo kiongozi wa baraza la seneti Mitch McConnell ameonyesha hali ya maridhiano akidokeza kuhusu mfumo wa vyama viwili nchini humo.