TAKWIMU zinaonyesha kuwa ukame umekuwa na madhara makubwa katika mji mkubwa nchini Brazil wa Sao Paulo.
Dokta ANTONIO NOBRE ambaye ni Mtaalamu wa hali ya Hewa amesema vyanzo vya maji vinaweza kutoweka na kusababisha madhara kwa zaidi ya watu Milion 20 iwapo hali hiyo ya uharibifu katika msitu wa Amazon hautadhibitiwa.
Baada ya kuwa ndani ya ukame kwa zaidi ya miaka nane mfululizo kina cha maji kwa sasa mjini Sao Paulo kipo katika hali ya hatari.
Serikali nchini humo imesema kuwa imelazimika kuanzisha mgao wa umeme kutokana na uhaba wa maji ikiwa ni moja ya hatua za dharula