JESHI la polisi mkoa wa Kipolisi Temeke limesema kuwa wanatarajia kufanya mkutano mkubwa na wamiliki wa nyumba za kulala wageni zilizopo katika mkoa huo ili kuweka mikakati mbalimbali ya kuzuia mauaji ya wanawake yanayotokea katika baadhi ya nyumba hizo.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kipolisi Temeke Kehenya Kehenya wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Amebainisha kuwa wanawake hao waliuwawa katika matukio tofauti na vifo vyao wote vimefanana kwani wameuwawa kwa kunyongwa shingo hivyo amewataka wamiliki hao wachukue taarifa kumbukumbu sahihi za wateja wao.