DONDOO ZA FORMULA 1 – LANGALANGA

DONDOO ZA FORMULA 1 – LANGALANGA

Like
324
0
Monday, 10 November 2014
Slider

FORMULA 1 – LANGALANGA

Dereva wa timu ya Mercedes Nico Rosberg apunguza tofauti ya alama katika msimamo wa mashindano ya langalanga (Formula 1) baada ya kuibuka kidedea kwenye mashinadno ya huko nchini Brazil (Brazilian Grand Prix).

Raia huyo wa nchini Ujerumani mwenye upinzani mkubwa na dereva mwenzake Lewis Hamilton ilimchukua saa moja dakika thelathini na sekunde mbili ikiwa ni ushindi wake wa tano msimu huu.

Hamilton anaongoza msimamo wa mashindano hayo akiwa na jumla ya alama 334 dhidi ya Rosber mwenye alama 317 atatangazwa kuwa bingwa wa mwaka huu kama atamaliza japo nafasi ya pili katika mashindano ya mbio za Abu Dhabi.

Endapo Nico Rosberg ataibuka mshindi wa masindano yam bio hizo za Abu Dhabi mnamo tarehe 23 mwezi huu na Hamilton akamaliza nafasi ya tatu au zaidi ya hapo, Rosberg atatangazawa kuwa bingwa wa michuano ya Formula 1 mwaka 2014.

Comments are closed.