TENNIS
Pazia la michuano ya ATP World Tour limefunguliwa rasmi hapo jana usiku katika viwanja vya O2 huko jijini London nchini England.
Andy Murray anayetokea katika visiwa hivyo vya Uingereza amejikutan akipokea kichapo kikali cha seti 6-4 6-4 kutoka kwa MJapan Kei Nishikori ambaye ni mara yake ya kwanza kushiriki katika michuano hiyo ya kufunga mashindano ya mwaka.
Kichapo hicho kinamuweka Murray katika wakati mgumu sana ndani ya kundi B linalojumuisha mchezaji bingwa namba mbili duniani, Roger Federer anayeshikilia rekodi ya kutwaa mataji mengi katika historia ya michuano hiyo.
Wakati huohuo MCanada Milos Raonic amepoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Federer kwa seti 6-1 7-6 (7-0). Mechi nyengine za kundi hilo zitapigwa siku ya jumanne kwa kuwakutanisha Murray vs Raonic huku Federer vs Nishikori.