Kiungo wa kimataifa wa Brazil Oscar Dos Santos Emboaba Jr. asaini mkataba wa miaka mitano ndani ya klabu ya Chelsea utakaomfunga ndani ya Stamford Bridge mpaka mwaka 2019.
Oscar alijiunga na Chelsea msimu wa mwaka 2012 akitokea klabu ya Internacional kwa dau lililoripotiwa kuwa ni kiasi cha paundi million 20 chini ya utawala wa kocha Di Matteo.
Chelsea inayonolewa na kocha Jose Mourinho imekuwa katika kiwango kizuri sana msimu ikiwa inaongoza ligi kuu nchini England bila ya kupoteza mchezo wowote mpaka sasa kwa kupata alama ishirini na tisa, alama nne juu ya Southampton inayoshika nafasi ya pili.
Wachezaji kama Diego Costa, Cesc Fabregas na Eden Hazard wamekuewa wakitajwa kuwa msaada mkubwa ndani ya kikosi hicho ila Oscar na Nemanja Matic wamekuwa wakifanya kazi kubwa sana ya kupora mipira kutoka kwa wapinzani.