NOVAK DJOKOVIC AMCHAKAZA MIRIN CILIC MICHUANO YA ATP WORLD TOUR

NOVAK DJOKOVIC AMCHAKAZA MIRIN CILIC MICHUANO YA ATP WORLD TOUR

Like
377
0
Tuesday, 11 November 2014
Slider

TENNIS

Bingwa namba moja katika mchezo wa Tennis, Novak Djokovic ameanza vizuri michuano ya ATP World Tour kwa kumchakaza bingwa wa michuano ya wazi ya Marekani (US OPEN), Marin Cilic kwa seti 6-1 6-1 huko O2 Arena jijini London.

Djokovic anayesaka taji la tatu mfululizo katika michuano hiyo ikiwa ni rekodi iliyowekwa mara ya mwisho na aliyekuwa kocha wa Andy Murray, Ivan Lendl ilimchukua Mserbia huyo dakika 56 tu kuweza kumpoteza mpinzani wake raia wa Croatia.

Katika mchezo mwengine wa kundi A uliwakutanisha bingwa wa michuano ya wazi ya Australia, Stanislas Wawrinka dhidi ya Tomas Berdych ambapo raia huyo wa Uswisi alimsambaratisha Berych kwa seti 6-1 6-1 mchezo ulioelemea upande mmoja kwa kipindi kirefu.

Matokeo hayo yanawaweka pazuri Djokovic na Wwarinka huku mchezo unaofuata utawakutanisha miamba hii miwili na mshindi ataweza kukata tiketi ya kutinga nusu fainali.

Comments are closed.