WANNE WAUAWA KWA VISU KENYA

WANNE WAUAWA KWA VISU KENYA

Like
293
0
Tuesday, 18 November 2014
Global News

WATU wanne wameuawa kwa kuchomwa visu na vijana waliokuwa wamejihami mjini Mombasa Pwani ya Kenya.

Watu kadhaa pia wamejeruhiwa katika shambulio hilo la usiku wa kuamkia leo kwenye vituo vya basi Kisauni. Bado haijajulikana waliouawa lakini inaaminika walikuwa raia wa kawaida waliokuwa kwenye shughuli zao.

Aidha inadaiwa vijana hao walikuwa wameziba nyuso zao, wakipeperusha bendera nyeusi sawa na ile iliyopatikana katika msako wa jana kwenye misikiti ya Musa na Sakinah, jijini Mombasa.

 

Comments are closed.