ASILIMIA kubwa ya wakazi wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma hawatumii vyoo vya kudumu hali ambayo inahatarisha usalama wa afya zao.
Uchunguzi uliofanywa na EFM katika baadhi ya vijijivya Wilaya hiyo umebaini kuwa wananchi wengi wanatumia vyoo vya muda ambavyo siyo salama hasa kipindi cha Mvua kwani vimejengwa kwa nyasi bila kuezekwa.
Vijiji ambavyo wananchi wake wanatumia vyoo vya muda ni pamoja na Luegu, Nahoro, Ukiwayuyu, Ngwinde na Namanguli