UGANDA: USHAHIDI WA VIDEO WABADILI KESI KUWA JARIBIO LA MAUAJI

UGANDA: USHAHIDI WA VIDEO WABADILI KESI KUWA JARIBIO LA MAUAJI

Like
313
0
Monday, 24 November 2014
Global News

POLISI Nchini Uganda wamebadilisha mashtaka ya mfanyakazi wa nyumbani aliyenaswa kwa kamera akimpiga na kumtendea unyama mtoto wa mwaka mmoja na nusu, kutoka kosa la kutesa na sasa anakabiliwa na kosa la jaribio la mauaji.

Video hiyo iliyowaudhi watu wengi kwenye mitandao ya kijamii lakini baba wa mtoto huyo amesema walisambaza video hiyo ili kuwatahadharisha wazazi wengine.

Mfanyakazi huyo wa nyumbani Jolly Tumuhirwe, alikuwa amezuiliwa katika gereza la Luzira na mahakama ya Nakawa kwa kosa la kutesa chini ya kifungo cha 41 kwenye katiba kinachoongelea dhidi ya mateso.

Mwanamke huyo sasa anatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 8 Disemba.

Hata hivyo, msemaji wa polisi Bwana Fred Enanga, amesema shtaka dhidi ya mwanamke huyo lilibadilishwa baada ya kupitiwa na mwendesha mkuu wa mashitaka.

Tumuhirwe alikubali kosa la kumpiga mtoto huyo, tuki olililonaswa kwa kamara ya CCTV. Polisi walimfanyia Tumuhirwe uchunguzi wa kiakili na kubaini kuwa ana akili timamu.

http://youtu.be/n3UcjCzavOU

 

Comments are closed.