KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Papa Francis amelitaka bara la Ulaya kutayarisha sera moja na ya haki katika suala la uhamiaji.
Amesema mamia kwa maelfu ya wahamiaji wanaowasili katika mataifa hayo kila mwaka kupitia baharini wanahitaji kukubalika na msaada, na sio kuwa na sera zenye maslahi binafsi ambazo zinahatarisha maisha na kuchochea mzozo wa kijamii.
Papa Francis ametoa kauli hiyo katika bunge la Ulaya wakati wa ziara fupi iliyokuwa na lengo la kuelezea mtazamo wake kwa Ulaya robo karne baada ya Papa John Paul wa pili kuzuru Strasbourg na kulihutubia bara ambalo bado limegawanywa na pazia la chuma.