RAIS wa Ufaransa Francois Hollande anatarajia kuanza ziara yake nchini Guinea kesho, itakayomfanya kuwa kiongozi wa kwanza wa magharibi kuitembelea nchi iliyoathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa hatari wa Ebola.
Guinea tayari imewapoteza watu 1,200 kutokana na ugonjwa huo, ambao kufikia sasa umewaua zaidi ya watu 5,600 na kuwaambukiza wengine 16,000 hasa katika eneo la Afrika Magharibi, kwa mujibu wa Shirika la Afya ulimwenguni – WHO.
Katika hatua nyingine Watafiti wa chanjo ya Ebola nchini Marekani wamesema kuwa wametiwa moyo na matokeo ya awamu ya kwanza ya majaribio ya chanjo ya ugonjwa huo.