MFANYAKAZI za Ndani wa Uganda ambaye alinaswa kwenye kanda ya video akimchapa na kumkanyaga mtoto mdogo amepatikana na hatia ya ukatili na hivyo atafikishwa Mahakamani siku ya Jumatatu Disemba 15 mwaka huu.
Jolly Tumuhirwe ameiambia Mahakama kuwa alilazimika kufanya kitendo chake kwa sababu mamake mtoto huyo aliwahi kumchapa mara kadhaa.
Hata hivyo waandishi wa habari wamezungumza na mama wa mtoto aliyefanyiwa ukatili huo ambaye amekanusha madai ya Jolly akisema hajawahi kumgusa Jolly hata wakati mmoja huku akihoji madai ya Jolly akisema angewezaje kumchapa msichana huyo wa kazi na kisha amuache na mtoto wake.
Huenda Tumuhirwe akafungwa jela miaka 5 kwa kumchapa na kumjeruhi mtoto.