Mwimbaji mwenye umri wa miaka 26 kutoka Marekani Rihanna kwa sasa yupo huko Herzogenaurach, nchini Ujerumani kumalizia dili alilopewa na kampuni ya Puma kuwa balozi mpya wa kimataifa wa bidhaa za michezo za Puma
Rihanna atakuwa mkurugenzi kwenye idara ya ubunifu kwa upande wa wanawake atakaeanza kutoa mafunzo kwa jamii mapema mwakani, mkataba huo utadumu kwa miaka kadhaa
Kupitia mtandao wa Instagram Rihanna alishea picha akiwa amevaa baadhi ya bidhaa za Puma kama sehemu ya kutangaza bidhaa hizo