RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameidhinisha sheria mpya ya usalama ambayo inawezesha majasusi kunasa mawasiliano kisiri au kufanya udukuzi pamoja na kuwazuia washukiwa wa ugaidi kwa mwaka mmoja kabla ya kuwafungulia mashitaka.
Kenyatta amesema kuwa sheria hiyo mpya inahitajika kwa ajili ya kukabiliana na tisho la ugaidi kutoka kwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab.
Amesisitiza kuwa sheria hiyo haikiuki haki za binadamu wala kuwapokonya watu uhuru wa kujieleza.
Hapo jana, wabunge wa serikali na wa upinzani walipigana makonde bungeni wakijadili marekebisho kwa mswada kabla ya Rais kuupitisha kuwa sheria. Katika vurugu hizo mmoja wa wabunge wa upinzani alimmwagia maji naibu spika.