WAGOMBEA URAIS nchini Tunisia wamebishana juu ya matokeo ya uchaguzi wa Duru ya pili uliyofanyika hapo Desember 21 mwaka huu.
Mwanasiasa wa muda mrefu BEJI CAID ESSEBSI amedai kushinda, lakini mpinzani wake, ambaye ni Rais wa sasa MONCEF MARZOUKI amekataa kukubali kushindwa.
Matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa hii leo, huku Bwana ESSEBSI mwenye umri wa miaka 88 anaaminika kushinda asilimia 54 ya kura, akiwa mbele ya Bwana MARZOUKI kwa asilimia 10.