PAKISTAN imewanyonga wapiganaji Wanne wenye Itikadi Kali za Kiislamu, baada ya kuondolewa marufuku ya kutolewa adhabu ya kifo katika kesi zinazohusiana na ugaidi.
Watu hao ni kundi la pili la watu walionyongwa tangu kundi la Taliban lilipofanya mashambulizi na kuwaua zaidi ya watu 140, wengi wao wakiwa watoto kwenye shule moja ya jeshi mjini Peshawar.