WASICHANA zaidi ya 100 wamepokelewa katika kituo cha Mpango Serengeti Tunaweza Bila Ukatili wa Kijinsia,HIV Aids na Ukeketaji.
Mratibu wa Mpango huo RHOBI SAMWEL amethibitisha hilo kwa njia ya Simu wakati akiongea na EFM Wilayani Serengeti mkoani Mara.
Amesema Wasichana hao wamepokelewa kuanzia Desember 6 mwaka huu ambapo wamekimbia kukwepa msimu wa Ukeketaji ambao hufanyika kila mwaka.