WAKAZI WA KIMARA BARUTI WAMO HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MRIPUKO

WAKAZI WA KIMARA BARUTI WAMO HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MRIPUKO

Like
346
0
Friday, 26 December 2014
Local News

WAKAZI WA KIMARA Baruti Jijini Dar  es salaam wapo hatarini kukumbwa na Magonjwa ya Mripuko baada ya eneo wanalohifadhia taka  kujaa.

Wakizungumza na EFM wakazi hao wamesema kuwa hapo awali walikuwa wakiweka taka hizo katika magari ya kuzolea taka lakini cha kushangaza magari hayo hayapiti hali inayowapelekea kukaa na taka hizo majumbani huku wengine wakizipeleka eneo la kilungule kwa ajili ya kutupa.

Wameeleza kuwa tarari wameshatoa taarifa kwa Uongozi wa Serikali ya Mtaa ili kutatua tatizo hilo lakini cha kushangaza mpaka sasa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa ili kuweza kumaliza tatizo hilo.

Comments are closed.